KONA YA UTAMU: November 2016
Breaking News
Loading...

Wednesday, November 30, 2016

Hatua Za Kufanya Kama Mwanamke Hataki Kujibu Texts Zako

Image result for TEXTING
Unafukuzia mwanamke mzuri mnaanza kuzungumza. Mnachukua muda wa dakika 20 hadi 30 kuongea na yeye mara ya kwanza. Anapendeza na kuvutia, na unaona kama ni mwanamke ambaye ni yule aliyekuwa ndotoni mwako maishani mwako. Mazungumzo yenu yanaenda vizuri mpaka ukwamwomba namba yake.

Baadaye unajaribu kumtumia text na hazijibu. Labda mnaeza kuchat kwa madakika halafu baada ya hapa anakataa kujibu texts zako. Unabaki ukijiuliza maswali ni kitu gani ambacho umefanya ambacho umekosea. Ok labda anaweza kuwa yupo buzy unampa muda kiasi ajibu text zako...unangojea masaa, siku, wiki mpaka inafikia wakati unagundua kuwa amekupuuza. Kwa nini hajajibu text zako?

So kwa nini hakujibu text zako?
Katika situation nyingi ni kuwa sababu kuu ambayo amekataa kujibu texts zako ni kuwa haukumpendeza mara ya kwanza ulipokutana naye. Ok labda sababu nyingine inaweza ni kuwa ameibiwa simu yake wakati alipokuwa akitext na wewe barabarani ama kitu kingine kama hicho, lakini hapa acha tumakinike na hatua ya kwanza uliokutana naye...yaani first impression ambayo unakudana na mwanamke yeyote.

1. Hakikisha unampendeza mara ya kwanza unapokutana naye
Anaweza kuwa hana muda mrefu wa kukaa na wewe ili akutambue zaidi so kile kitu ambacho unahitaji kufanya ni kuwa lazima uuonyeshe upendo wako kwa kuwa mpole, mkarimu na mtulivu. Hii itamfanya yeye kumakinika na labda kutaka kukufahamu. Hakikisha kuwa wakati unapoongea na yeye tumia mbinu za kuonyesha kuwa ungependa kukutana na yeye wakati mwingine. Kama hakuonyesha dalili zozote za kukuelewa basi hata kama atakupatia namba yake ya simu fahamu ya kwamba itakuwa ni kazi bure.

2. Taja sababu zako za kuongea na yeye
Mfano: Nimefurahia sana kuongea na wewe. Kusema kweli nimependa maonezi yetu machache. Nataka kwenda lakini naonelea wikendi nitakutext tukutane ili tuongee tena. Hapa utakuwa umeeleza ajenda yako kwake hivyo ukianza kuchat na yeye baadae haitakuwa vigumu kwake kukujibu.

3. Hakikisha kuwa unamtumia text wakati ufaao
Ukiomba namba ya simu kwa mwanamke inamaanisha kuwa wewe umeonyesha intrest kwake vilevile mwanamke akikupatia namba yake ya simu inamaanisha kuwa labda itakuwa amependezwa na wewe. Lakini je, ni muda upi unaotakikana hadi umtext mwanamke huyo.

Wanawake wanapenda kuona wanababaikiwa na kufukuziwa. So usijaribu kumtext hapo hapo wakati amekupatia namba yake. Hakikisha umejibatia shughli nyingi ili usahau kabisa kama uchukua namba kwa mwanamke. Masaa mazuri ambayo yangekuwa sawa ya kumtext ni baada ya masaa 24 baada ya kuchukua namba yake. Hii itamfanya mwanamke yeyote kujiuliza maswali ya kwa nini umechukua muda mrefu kumtext. Itamfanya kuingiwa na maswali ya kama: kwani hajapenda chat yangu? yuko na mwingine? nk. Ukichukua muda huu mrefu hadi kumtext, itakuwa rahisi kwake kukujibi.

ONYO: Hakikisha ya kwamba haupitishi zaidi ya siku tatu kwani anaweza kukusahau kwa haraka ama kuona unampotezea wakati wake.

4. Kitu cha kuandika kwa text yako ya kwanza
Messages za kwanza ambazo utazituma kwa mwanamke zitachangia pakubwa kuona kama wewe uko uko interesting ama unaboa. Unaweza kuuharibu mchezo mzima kama iwapo utaanza kumtext na mambo ambayo hayana manufaa kwake. Kile kitu unachohitajika kufanya hapa ni kuonekana hauna haraka na ujaribu kutumia lugha za kirafiki. Mfano unaweza kujaribu kumtext swala ambalo aliligusia kwa chat iliyopita. Labda aliongea kuhusu kwenda shopping na nduguyake, so swali lakini linaweza kuwa: Je ile shopping yenu na nduguyako iliendaje?. Hii itamfanya kuwa interested na wewe manake ataona ya kuwa ulikuwa umemakinika wakati mlipokuwa pamoja. Hii itamfanya kujibu text zako mara kwa mara bila yeye kuchoshwa.

5. Jaribu kuhepa stori ambazo hazitafikia popote
Mara ya kwanza anaweza kukujibu lakini itafikia pahali atanyamaza. KUMBUKA: Siri kuu ya kumfanya mwanamke ajibu texts zako ni uwe makini kwake, yaani unamtext vtu ambavyo unajua yuko intrested navyo.

6. Weka wazi kuwa unataka mkutano
Acha stori za kumzungusha huku na huku kama wanaume wengine. Ukitaka akujibu text zako hakikisha ya kuwa unadhihirisha azma yako kwa kumwambia kuwa unataka kukutana naye.

7. Usikate tamaa
Kuna wanaume wengine kama wamekataliwa kujibiwa texts zao mara moja basi wanakasirika na wanaachana kabisa na kushungulika tena. Tatizo labda linaweza kuwa mwanamke anakupima akili aone bidii yako kwake. Kama tujuavyo tabia za wanawake ni kuwa hawapendi kuonekana kama ni watu wa kukubaliana na kila kitu hivyo basi wakati mwingine wanakuwa hawaeleweki.
Ukiona mwanamke amekataa kujibu text yako kwa siku tatu, fanya kumtext tena huku ukionyesha kuwa hauna intrest naye sana vile halafu achana naye. Hii itamfanya yeye kuona una interest na yeye lakini hauna haraka. Baadaye anaweza kuanza chat yeye mwenyewe.
KUMBUKA: Kuna sababu tofauti tofauti ambazo zinaweza kumfanya mwanamke kukataa kujibu texts zako. Labda umemtusi, hujampendeza, ni mwanamke mwenye haya nk. So hizi hatua zitategemea na vile imetokea katika situation yako.
 
Pata mchumba, mpenzi! Click Hapa

Karibu sana msomaji wangu kila siku upate mbinu mbali mbali za kukuondolea aibu katika mahusiano yako. Ukijenga utamaduni wa kutembelea mtandao huu kila siku muda si mrefu unakuwa tajiri wa mahaba pamoja na kuwa na mahusiano thabiti sana. Kazi kwako!

 

Msaada jamani, Kwani ni lazima kumbebeleza mwanamke?

Kuanzia utotoni na hadi maisha ya shule nimekua katika hali ya kuyapeleka maswala yangu haraka haraka kadri ninavyotaka mimi. Katika style hiyo ya maisha imenipa faida na maendeleo mazuri.

Lakini aina hiyo ya maisha sikuwahi kabisa kumshawishi mwanamke tukaingia naye mahusiano. Nilijaribu kuwashawishi lakini walikataa wengine waliniahidi ahadi hewa. Hali hiyo haikunishutua kabisa, wasichana walionindaganya na kunikataa niliwapuuza na kuwaona ni wajinga tu. Kwani mimi nilijiona ni mume mzuri wenye kila sifa.

Na zaidi ya yote nilipohisi hali ya kufanya mapenzi nilienda kununua makahaba na kupiga masturbation. Kwa kweli katika ulimi na kinywa changu sina kabisa maneno ya kubebeleza mtu.

Maswala sasa yanakuwa magumu sana kwani hahitaji mke wa kuoa ili na mimi ni maisha yawe kama wengine na kuwa na mwanamke anayenipenda kwa hiyari yake.

Kila mwanamke ninayemfata nikajaribu kumweleza kumuoa analeta mapozi na kukataa hali ambayo inayonifanya kukataa tamaa. Na nafsi yangu huniambia huwezi kukaa ukimubebeleza mtu.

Wanawake ambao mpo humu JF naomba mnieleweshe, kwani ni lazima mbebelezwe na mpewe maneno matamu ambayo mengi ya maneno hayo ni uongo?
 

Nimetokea kumpenda sana hadi nashindwa kujicontrol

Wadau,

Nina kadent kangu ka 1st yr chuo flani hivi, haka kabinti nina muda nako naeza kukadiria ka 3 yrs.

Ofcuz kenyewe ndio kalifall in-love kipindi hiko mimi nipo college nilikua nakadharau. Sasa siku hizi kamekua M' SUPER ni kazuri kinyama.

Wakuu naeza sema kataniua kwa presha, mzee nimekuja kujikuta nina malengo nako yale ya mbalii kichizi plus na kumpenda basi ni hatarii tupu.

Somtimes naeza kukapigia simu nikakuta inatumika basi nitazila hapo, nitafikiria na mimi kulipiza kisasi cha kumpigia mtu mwingine maana najua katanicall back si nako kananipenda.

Wazee kataniuaa haka katoto nikienda nako na speed hii ambayo zamani sikua nayo.

Ushauri tafadhali.
 

Mimi black na mke wangu black mtoto kazaliwa na nywele za kiarabu

Nisaidieni wataalamu,

Hii ni siku ya tatu toka mtoto huyu azaliwe na nywele za kiarabu, leo kaja mama mkwe wamemnyoa kabla ya siku saba, nipo kimya muda wote kwa kuwa mke wangu ni mfanyakazi hawajaniomba chochote, mama yangu mzazi kafika nimemchungulia dirishani naona anamkagua sana kwa siri vipi hakuna.

DNA YA BEI RAHISI NIMALIZE FITINA.

Nioe yupi kati ya hawa? Nishaurini


Bila shaka wazima.

Kijana wenu/mwenzenu nina tatizo moja sielewi nini cha kufanya
Nilikuwa na mpenzi wangu mmoja tulipendana sana na bado nampenda sana na yeye namsifu anajua kuhandle penzi japo mapenzi yetu yameyumba kidogo kwa sasa.

Matatizo kwa kipindi chote nilichokuwa nae kiukweli (on bed) hawezi kumudu goli tatu katika tendo la ndoa, goli moja tu hataki tena na nikifanya masihara naweza kumalizia na mkono (ny*to), siwezi kulaumu kama tatizo ni yeye au mimi nakawia ku-pees, alafu kuna style ninayoipenda ya kuchuma mboga ambayo niki apply hiyo angalau nawahi kukojoa japo yeye haipendi anadai inamuumiza kizazi.

Navumilia kwa sababu nampenda siku moja nilikaa nikawaza nikasema wacha ni jaribu kutafuta mchepuko nione tatzo nini, kweli nikapata mchepuko nako yakanikuta majanga zaidi japo tofauti na ya yule ambae nampenda, nilikuwa katika majaribio lakini nikajikuta mapenzi yameamia kwake sio siri ni yupo vizuri ila dini tofauti na amenipenda sana alafu nilimdanganya sina mtu na yupo flexible kwa sexy style zote so naenjoy sana nikifanya nae mapenzi nalidhika 100%, nayeye amekubali show yangu kiasi kwamba nayeye beki hazikabi.

Mimi binafsi moyo ukawa umebeba mapenzi ya watu wawili nikiamini hawatokaa wafahamiane na isitoshe wote wakawa wanaupendo wa dhati kiasi cha kuolewa na mimi leo kesho, mwenendo huo hatukumaliza miezi mi3 mpenzi wangu wa awali akagundua kuwa nna mtu mwingine, siku simu yangu ilipigwa usiku wa kama saa tano ikapokelewa na mpenzi wangu (ni kawaida kupokea simu yangu hapo awali tuliaminiana sana kiasi cha kuwa free na simu so nikashindwa kumzuia) akakutana na sauti ya kike ghafla simu ikakata kwa kuchukia kwanini apokee mwanamke then akautuna msg akilalamika sana alaf anatabia ya kuniita mume japo hatujafunga ndoa ,
Ugomvi ukaanza hapo huyu anasema huyu nan anpiga simu usiku na anakuita mume ?

Kiukweli nilikosa majibu coz sipo vizuri kwa kujitetea kwa vitu kama hivyo ila niliyamaliza yakaisha japo hakuwa na imani tena na mimi maana dalili aliziona (mawasiliano yalipungua sana, kukutana hakukuwa kama awali ilivyokuwa hazipiti siku mbili either aje alale kwangu au nikalale kwake kibaya zaid siku akaja kwangu akakuta picha yake nillibandua ukutani bila sababu ya msingi kwake ila nilifanya hivyo ili yule mwingine asigundue lolote inshort nilielemewa na mapenzi yake so sikuwa tayari kuudhi yoyote kati yao maana kila mmoja alikuwa ana nafsi yake katika moyo wangu, mapenzi automatically yalishuka upande mmoja) na huyu mchepuko nikayamaliza akanisamehe.

Sasa nifanyaje waungwana nimejaribu kuifupisha maana visa vingi sana katikati nisiwachoshe ila kiukweli nampenda wa kwanza kwa tabia dini yake isipokuwa mapenzi (kwichikwichi zero) na mchepuko dini tofauti japo yupo radhi kubadili dini na mapenzi anayajua, ila upendo haufikii yule wa kwanza nifanye nini wadau (nata mke wa kuoa katika hao.)

NB; Mitara sitaki japo ni dini yangu inaniruhusu.

Shukrani.

Ukiona mwanaume ana vitabia hivi muepuke haraka sana

Image result for wivu wa kimapenziHabarini wapendwa,ukiona upo katika mahusiano na mwanaume mwenye vitabia kama hivi,anapenda sana kujikweza,muda wote anakuhisihisi kuwa unamsaliti kimbia ujue hiyo ndo tabia yake hivo anakuhisi na wewe,ana vijimanenomaneno vya kike,ukikaa nae anapenda kujadili watu flani kafanya hivi flani kafanya vile ujue sio,ukimkosea akikusamehe daily anakumbushia kosa ulilofanya,anapenda muda mwingi muwe mnachati tu kama hakuna majukumu mengine ya kufanya,mara kwa maraanauliza uliza sana kuhusu ex boy wako the way alivokua anakufanyia mkiwa bed yani ujue hajiamini then tangu uwe nae katika mahusiano hakuna siku ameongelea kuhusu michakato ya kuzisaka pesa na kuongeza kipato yeye analalamika tu kwamba maisha magumu pia ukiwa na man ambaye ukiwa na shida ya pesa hajawai kutimizia yeye kila siku sina hela sina hela utafikiri ndo ubini wake,mwanaume wa hivo muepuke kama ukoma sababu hafai kuwa nae katika mahusiano sababu anakua amejaa ubinafsi,kutokujiamini ukiwa nae always utapata vitu negative tu forget about positive.

Tuesday, November 29, 2016

Changamoto ya kuoa msichana mrembo sana wa kuvutia au mwenye akili sana asiyevutia

Image result for umbo namba nane
Wakuu sijui kama uzi huu umewahi kutolewa. Mara kadhaa naulizwa ushauri, inapotokea kijana wa kiume anataka kuoa kati ya msichana mrembo mwenye umbo la kuvutia sana, yaani ukitoka naye kila mwanaume atageuka kumtizama kwa kumhusudu. Ukimwona kavaa vizuri lazima usisimke mwili. Tatizo msichana mwenyewe kichwani ni mtupu sana. Mara nyingine anaongea mambo au kuuliza maswali utafikiri hajasoma, japo ana diploma ya marketing.

Upande wa pili anakuwapo msichana ambaye kwa kweli kwa sura na maumbile sio yule wa kutisha wala kushitua. Ana digrii ya BA education. Yupo kawaida sana, na sio wa kusema atakusisimua sana mwili hata kama amevaa kivipi. Na pia ana tatizo la kujipenda, ila sio mchafu, ni msafi sana tu. Kwa ujumla sio msichana wa kusema wanaume watageuka kumwangalia tena wakipishana naye au mkiwa pamoja. Ila sasa, ukiongea naye, kwa hekima na busara na kujishughulisha na kazi nyumbani yaani hakuna mfano wake. Anatoa mawazo ambayo inaonyesha anafikiri kabla ya kuongea.

Sasa huwa naulizwa; kati ya aina mbili hizi za hawa wasichana, ungechagua yupi umuoe na kuishi nae maisha yako yote; akili au urembo?

Ananiambia bikira yake imeyeyuka!

Image result for bikra
Salaam!
Habari wana kona ya utamu poleni na majukumu, mimi ni kijana ambae nimepanga kuoa mapema mwakani ila leo mchumba wangu kanitumia ujumbe unaonivuruga akili,
Kiukweli mimi na mchumba wangu hatujawahi kushiriki tendo la ndoa na alinihakikishia kuwa yeye ni bikra lakini leo kanitumia ujumbe ana wasiwasi kuwa bikra imetoka kutokana na kuhisi maumivu mara kwa mara na kazi ngumu anazofanya,

Naombeni wajuzi mnisaidie ni kweli sababu alizotoa zinaweza kusababisha bikra itoke!?

Mimi nilichomuambia bikra ikitoka asahau kuhusu ndoa!

Masharti Ya Kumtext Mwanamke - Makosa 5 Unayoyafanya

Image result for textingKila siku mara moja au nyingine huwa tunawatext wanawake. Aidha wawe ni wapenzi wetu, tunaowatongoza ama marafiki zetu. Na kila siku huwa tunapatwa na changamoto mbalimbali kutokana na matangamano yetu. So huwa kunakosekana nini? Ifuatayo ni orodha ya mambo 5 makuu ambayo wanaume wengi hukosea wakati wanapomtext mwanamke, na jinsi ya kutatua.
Zama nasi...

#1 kukata tamaa mapema kwa mwanamke
Kosa kuu ambalo wanaume wengi hufanya ni kukata tamaa mapema wakati wanapomtext mwanamke. Watamtext mwanamke, na kama hatajibu jumbe zake (ama kujibu kiuchache) watachukulia kuwa mwanamke huyu amepoteza interest na wanakata tamaa. Hili ni kosa kuu sana.

Kama inavyojulikana kikawaida ni kuwa mwanamke anaweza kutojibu meseji zako, na sababu hizo hazina uhusiano moja kwa moja na kutokuwa na interest kwako. Kwa mfano, anawezakuwa labda yuko busy, katika mood mbaya, ama labda hayuko sure ni kitu gani cha kukujibu kwa meseji. Kiufupi ni kuwa haujui kile ambacho kinazunguka kwa akili ya mwanamke, so haina haja ya kufikiria jambo baya.

So, iwapo kama mwanamke hakukujibu ama hayuko interested na wewe, lakini bado unataka kuongea na yeye, hivi ndivyo unavyopaswa kufanya; Mpe muda wa kutosha (siku chache ama hata wiki) halafu anza kumhusisha kwa meseji. Kama vile texts zozote za kawaida, hapa utakuwa unataka kuhakikisha kuwa unamvutia, unamfurahisha na unamchesha. Na zaidi ni kuwa unapaswa kutafuta swali ambalo litamlazimu yeye kureply meseji yako. Yote hayo, huu hapa ni mfano mzuri wa meseji ambayo itamhusisha mwanamke yeyote:

Hello mrembo...hivi kweli uko hai? Nitume kikosi cha maninja kije kikunusuru ama?

Yaweke maneno yako kuwa ya ucheshi, yawe na kamchezo flani na bila shaka utamfanya huyu mwanamke kutabasamu na kuwa katika hali ya kuchangamka. Kama utaweza kumfanya atabasamu basi muda mchache tu atakujibu.

2. Kutext mara nyingi.
Hakuna kitu ambacho kinaweza kuua nafasi yako kwa mwanamke kama kumtumia jumbe mara nyingi. Humfanya mwanaume aonekane mwenye tamaa hivyo kumfukuza mwanamke.

Kwa kuepuka haya yote hizi hapa ni njia unazoweza kuzitumia ambazo zinaweza kukusaidia kumtext mwanamke wakati sawa.

♥Unapomtext mwanamke, hakikisha kuwa jumbe zinakuwa 1:1, Unahakikisha kuwa kila meseji anayotuma unaijibu na moja (pia hakikisha urefu unakuwa sambamba)

♥Acha kumtext na jumbe zisizo na mwelekeo. Usimjibu mwanamke jumbe wakati ambapo haihitaji jibu. Kwa mfano, si lazima uijibu text ya mwanamke ya 'usiku mwema' kama utamwambia 'nawe pia'. Ikifikia hatua hii mazungumzo yenu yatakuwa yameisha. Inachotakiwa kutoka kwako ni kuhakikisha kuwa jumbe ya mwisho inaisha kutoka kwake.

♥Weka fikra ya wengi. Wakati ambapo unamtext mwanamke mmoja, huwa kawaida unakuwa na mtazamo finyu wa kumfiria sana mwanamke huyu ukiogopa asikuache. Well, kutatua swala hili, lile unalotakiwa kufanya ni kuhakikisha kuwa katika akili yako weka ya kuwa una wanawake kadhaa ambao wanakufukuzia. Hii itakusaidia kuondoa uhitaji mwingi wowote.

3. Kuchukulia jumbe unazomtumia serious.
Kuna hali tofauti tofauti ya kuwa serious na mwanamke wakati wa mazungumzo lakini kutumia jumbe si moja wapo. Kujifanya kuwa serious wakati wa kumtext mwanamke kunachosha na hakuna mtu anapenda. Hivyo weka seriousness zako mbali kabisa na ulete hali ya ''nataka-tujuane-nawe''. Wakati unapomtext mwanamke, unapaswa kumakinika kuleta furaha.

Sasa, njia nzuri ya kuhakikisha kuwa unamfanya mwanamke anakuwa na shangwe wakati wote ni kwa kutumia 'emoticons'. Wanaume wengi wanajitenga kutumia emoticon wakidhania kuwa ni mambo ya wanawake, ukweli ni kuwa ni mambo ya wanawake na wanawake wanapenda kutumia emoticon. Pia zinasaidia kwa kuwa kile utakachokisema kwa kutumia emoticon mwanamke hatakipuuza. Hatobahatisha hisia zako kamwe kwa kuwa emoticon zinasaidia kupitisha ujumbe unaodhaminia. Na matokeo yake ni kuwa unaepukana na drama zozote zitakazojitokeza.

4. Kutotext wanawake wengi.
Wakati mwanaume anatext mwanamke mmoja, ni rahisi kwake kumaliza maongezi yake mapema kwa kuwa hana fikra pevu kama vile tulivyotangulia kusema awali. Kama unataka kuwa na fikra pevu na uwezo rahisi wa kutangamana na wanawake basi ni lazima uwe unatext wanawake wengi.

 [Soma: Jinsi Ya Kuukwepa Mtego Wa Kuwa na urafiki wa kawaida Na Mwanamke Unayempenda]

Kufanya mazungumzo mengi na wanawake wengi kunakupa ufahamu na mbinu pana za kuweza kuzungumza na wanawake. Ustadi huu utakuja wenyewe iwapo utajikita kuongea na wanawake wengi na tofauti tofauti katika meseji zako. So kinachohitajika kwako ni kutafuta namba za wanawake tofauti tofauti na uanze kuongea nao kupitia jumbe.

5. Tunasahau lengo kuu la kumtext mwanamke.
Wakati mwingine wanaume wanasahau kwa nini wanawatumia jumbe wanawake. Wanakita kuongea mambo ya mbele, nyuma na ovyo bila msingi wowote ule. Wanasahau ile taswira kuu ya kumtext mwanamke. Taswira kuu kama tujuavyo ni kuhakikisha unatoka deti na mwanamke huyu.

Lakini usichukulie kuwa kuchat na mwanamke kupitia texts imepangwa, la. Unapaswa kutumia mfumo ule wa kawaida wa kuleta ucheshi, mzaha nk, kama tulivyoelezea awali. Hivyo basi, mbinu zako za kumtext mwanamke lazima ziwe za kuvutia, za nakshi na ambazo zitaleta msisimko ndani yake. Kama utamtext mwanamke bila mpangilia ama lengo flani, basi bila shaka atapoteza hamu na kuenda zake.

Pata mchumba, mpenzi! Click Hapa

Karibu sana msomaji wangu kila siku upate mbinu mbali mbali za kukuondolea aibu katika mahusiano yako. Ukijenga utamaduni wa kutembelea mtandao huu kila siku muda si mrefu unakuwa tajiri wa mahaba pamoja na kuwa na mahusiano thabiti sana. Kazi kwako!

Hatua 10 za kumchagua Mchumba

Image result for mchumba
Wengi wamejikuta wakiitwa wahuni kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na makundi ya wanaume au wanawake. Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya mapenzi wanasema idadi kubwa ya wapenzi si kigezo sahihi cha kupima tabia ya mtu na kumhusisha na uhuni.

Watalaam hao wanataja safari ya kupata chaguo halisi la mwanaume/mwanamke wa maisha ndiyo inayowaponza wengi kiasi cha kujikuta wameingia katika kashfa ya kuwa na uhusiano na dazeni ya wapenzi.

Wanasema msichana/mvulana anayeingia katika uwanja wa mapenzi kwa kuwa na hisia za kufanya ngono, hukosa umakini wa nani anafaa kuwa mpenzi wake kutokana na kukosa elimu ya uhusiano kutoka kwa wazazi wake.

Kwa mantiki hiyo, bila upembuzi wa kina, mtu asiye na elimu ya jinsi ya kumpata mpenzi wa kweli hujikuta ameangukia kwa mwanaume/mwanamke asiyemfaa, ambapo baadaye huamua kuachana na huyo na kwenda kwa mwingine kujaribu bahati tena ya kupata penzi la kweli.

Zinatajwa zawadi, hitaji la kusaidiwa kimaisha, mvuto wa kimahaba na mazoea kuwa ni vichocheo vinavyowaangusha wengi kwenye mapenzi na wasiowafaa.

Ukweli ni kwamba mtu aliyenaswa kwa ‘ujinga’, huwa hakatwi kiu ya penzi na mwanaume/mwanamke asiye chaguo sahihi la maisha yake. Hivyo hufikia maamuzi ya kujiingiza katika uhusiano mpya mara 2,3,4,5 na kujikuta wakiambulia wanaume/wanawake wale wale wasio sahihi kwake.

Mwanamnke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Suzzy aliwahi kuniomba ushauri, akasema amechoka kuchezewa, maana kila mwanaume anayempata anakuwa si chaguo lake. Lakini kibaya zaidi kuachia ngazi au kutemwa huku akiwa tayari ameshafanya mapenzi na wanaume hao.

Nia ya swali lake ilikuwa ni kuniomba njia za kumtambua mwanaume mkweli bila kufanya naye mapenzi? Aliuliza hivyo huku akiwa na hoja kuwa wanaume wengi hawako tayari kuwa na uhusiano na msichana bila kufanya naye mapenzi na wakati huo huo huficha tabia zao chafu wakilenga kumnasa wamtakaye.

Binafsi nafahamu kuwa kuna wanawake/wanawake wengi ambao hujiingiza katika mapenzi kwa kutekwa na hadaa za mwili na kujikuta wanacheza mchezo wa kitoto wa pata potea.

Ni madhumuni ya somo hili kufundisha vigezo vya kumpata mwanaume/mwanamke halisi wa maisha, bila kufanya naye mapenzi. Njia hii ina faida kwa pande zote mbili yaani kwa mwanamke na mwanaume kwani kuacha au kuachwa bila kufanya mapenzi ni bora kuliko kuwa muonjaji, tabia ambayo huathiri kisaikolojia na ni hatari kwa afya.

Ifuatavyo ni njia ya kisaikolojia ambayo mwanamke anaweza kutumia kumpata mwanaume mwenye kumfaa bila kufanya naye mapenzi tena ni jibu sahihi la kuondokana na mchezo wa kubahatisha kwa wanaume wanaosaka wapenzi wa kweli na si taksi bubu ambazo mchana huweka namba za njano usiku nyeusi.

KWANZA- Ni ya mwanamke/mwanaume mwenyewe kujifahamu na kufahamu vigezo vya mpenzi anayemhitaji katika maisha yake. Ifahamike kuwa kila mwanaume ana wake na kila mwanamke anaye wake wa maisha pia. Hivyo asiyekufaa wewe anawafaa wengine, kinachotakiwa ni wewe kujitambua kwanza ili umtambue umtakaye.

Wanawake/wanaume wengi hawafahamu wanahitaji wapenzi wa aina gani, hivyo wanajikuta kama watu wanaoingia sokoni bila kujua wanataka kununua nini? Ndiyo maana wengi wameangukia kwa matapeli wa mapenzi, wakachezewe na kuumizwa moyo bure.

PILI- Ni kuketi chini na kuorodhesha vigezo stahili vya mwanaume/mwanamke unayemtaka. Baada ya hapo orodhesha tena kasoro za mwanaume/mwanamke unazoweza kuzivumilia na zile ambazo huwezi kuzivumilia kabisa. Hii inatokana na ukweli kwamba mwanadamu hajakamilika, ana upungufu wake.

TATU- Anza kumsaka kwa kutumia milango ya fahamu. Cha kufanya hapa ni kuruhusu macho yawaone wanaume/wanawake na kuwatathmini kwa maumbile yao ya nje na kisha kupata majibu kutoka moyoni juu ya kuvutia kwao ambako hutambulika kwa moyo kurithika na mwili kusisimka.

NNE - Kuanzisha safari ya kuchunguza tabia za nje na za ndani kivitendo. Hapa suala la ukaribu baina ya mwanaume na mwanamke linahitajika. Msingi unaotajwa hapa ni kujenga mazoea ya kawaida yasiyokuwa na masuala ya kimapenzi na ngono. Kutambuana, dini, viwango vya elimu, kabila na makundi ya marafiki ni mambo ya kuzingatia.

Katika uchunguzi huu mwanamke/mwanaume anayetafuta mpenzi hana budi kupitia na kumlinganisha huyo aliyempata na vigezo alivyojiwekea. Zoezi hili liendane na kuweka alama ya pata kila anapobaini kuwa mwanaume/mwanamke anayemchunguza amepata moja ya vigezo vyake. Lakini pia aweke alama ya kosa kwa kila kasoro anayoivumilia na ile asiyoivumilia.

TANO - Ajipe muda wa kutosha kati ya miezi sita na mwaka kumchunguza huyo mwanaume, kisha aketi chini na aanze kujumlisha alama za vigezo alivyovijiwekea na jinsi mwanaume huyo alivyopata au kukosa.

Ikibainika mwanaume aliyechaguliwa amepata zaidi ya nusu ya alama ya vigezo vilivyowekwa, basi ujue kuwa anafaa. Kuhusu alama chache alizikosa anaweza kusaidia kuzikamilisha polepole wakati wa maisha ya ndoa.

Lakini angalizo kubwa kabisa ni kwamba mwanaume/mwanamke akionekana kuanguka katika kasoro zisizoweza kuvumilia kwa zaidi ya alama tatu. Yaani kwa mfano ni mlevi, mwizi, muongo, mbishi na katika hizo kashindwa 3, huyu hafai, ni vema akawekwa kando kwani huwezi kubeba kero 3 kwa pamoja katika maisha.

SITA - Kusajili mapenzi yenye malengo yanayotekelezeka. Lazima baada ya kuchunguzana kwa kina wapenzi watengeneze muongozo wa mapenzi yao. Wasiwe kama wanyama, lazima mipango ya wapi wametoka walipo na wanapokwenda.

Hata hivyo watalaam wanasema lazima wapenzi wapime umakini wao kwa vitendo. Kama wamekubaliana kuoana, suala la mume kwenda kujitambulisha kwa wakwe na hatua ya kuiendea ndoa ionekane. Usiri usiwepo tena. Kila mmoja amuone mwenzake kama sehemu ya maisha yake na mara zote wasaidiane kwa ukaribu.

SABA - Ni vema ndugu wakashirikishwa ili kuwapa nafasi na wao ya kuamua kama mapenzi hayo ni budi yakaendelea au yakasitishwa. Ni ukweli ulio wazi kwamba licha ya wengi kupuuza maamuzi ya ndugu kwa madai ya kuwa hawana nafasi kwa wapenda nao, lakini uchunguzi unaonesha kuwa wapenzi wengi huacha kutokana na sumu za ndugu hasa pale wanapokuwa wameonesha kutounga mkono uhusiano wa wanaotaka kuoana

NANE - Hatua hii ni ya kuweza kuzungumzia ufanyaji mapenzi, hapa nina maana kama wapenzi wamejizuia kwa muda mrefu na wanahisi kuchoka wanaweza kujadiliana kuhusu hilo na kuamua ufanyaji huo wa mapenzi una lengo gani, kama ni kuburudisha miili basi suala la afya na uzazi salama litazamwe.

TISA - Kutimizwa kwa ahadi ya kuoana ni hatua ya tisa ambayo nayo si busara ikachukua muda mwingi kutekelezeka, kwani ucheleweshaji mwingi wa ndoa nao huvunja moyo na mara nyingine umewafanya wengi kutoaminiana.

KUMI - Kuamua kuwa mwili mmoja kwa kuvumilia na kuwa tayari kukabiliana na changamoto zote za maisha ukiwemo mkwamo na dhiki ambazo huchangia sana ndoa nyingi kuvunjika. Hapa pia ni wajibu wa wanandoa kuchukuliana udhaifu na kusaidia, kuwa tayari kujifunza na kujali zaidi upendo kuliko hisia za mwili ambazo wakati mwingine hudanganya na hivyo kumfanya mwanandoa asivutiwe na mwenzake.
Mwisho ni kwamba kanuni hizi huwafaa watu wazima mapenzi ya kitoto hayawezi kujenga misingi hii imara mara nyingi ni kudanganyana, kuharibiana maisha, kupeana mimba na maradhi.