Kujifundisha
jinsi ya kumuapproach mwanamke kwa mara ya kwanza si jambo gumu la
kufanya kama utafuata kanuni na masharti na kuyahifadhi baadhi ya
michongo kwa moyo. Michongo ni maneno ya kwanza ambayo mtu hutumia
kuanzisha maongezi na mwanamke.
Maneno
haya ndio mara nyingi hutumiwa na wanaume mara yao ya kwanza
wanapomshobokea mwanamke. Ukiitumia vizuri michongo itakupa wewe nafasi
ya kumvutia mwanamke kwa uharaka zaidi.
Ingawa
wanaume wengi hutegemea zaidi bahati ama kukosa, hauwezi kamwe kufaulu
kumridhisha mwanamke iwapo hujui kuipanga michongo yako vizuri pindi
unapokutana na mwanamke unayemzimia kwa mara ya kwanza.
Ok. Kukusaidia kujipanga vyema, tumeweza kuiorodhesha baadhi ya michongo iliyowazi na iliyofunge na jinsi ya kuitumia.
Aina ya michongo -wazi na fungeUnaweza
kumuapproach mwanamke bila wasiwasi kwa kutumia michongo aina mbili
-wazi na funge. Michongo ile mizuri zaidi inakuwezesha wewe kuonekana
kujiamiani, mcheshi na kuonekana mtu anayevutia zaidi kuwaliko wengine
walioko karibu nawe.
Ijapokuwa michongo
iliyowazi inahitaji mtu mwenye kujiamini kwa kiasi cha juu, michongo
funge inaweza kutumika na yeyote yule bora tu ufuate masharti ya
kuitumia.
Michongo iliyofungeAina
hii ya michongo ni rahisi kuitumia kwa mwanamke na si rahisi kwake
kuelewa kama unatumia maneno kama hayo ukiwa na ajenda fulani. Michongo
hii ni kuanzia matukio, kumsifu ama kuangazia mazingira. Kila aina ya
michongo hii ina manufaa yake na pia upungufu wake kiasi fulani
kulingana na mazingira ambapo yanatumika. [soma: Hatua za kufanya kama
mwanamke anakataa kujibu texts zako]
1. MatukioAina
hii ya michongo ni rahisi kuikumbuka na ukiitumia kwa mwanamke atakupa
atenshen yake automatic. Michongo hii hutumika ili kutaka atenshen ya
mwanamke kwa kujaribu kumuuliza maswali ambayo yanalingana na mazingira
aliyeko.
Baadhi ya aina ya michongo iliyofunge ni kama:
"Unaweza kujua wakati gani gari lingine la abiria linaweza kufika hapa?"
"Je unajua sehemu nzuri ambayo mtu anaweza kujiinjoy katika huu mji?"
"Nlikuwa nataka kuvuta sigara lakini kibiriti changu sikioni, naweza kuomba chako?"
"Nilikuwa sijamaliza kuandika maswali ya mwalimu kwa ubao, unaweza kunisaidia kitabu chako?"
2. KumsifuAina
hii ya michongo inakaribiana na ile ya wazi lakini kwa mpango flani
inazuia kumfanya mwanamke kuelewa ajenda yako kwa uharaka. Michongo hii
inafaa zaidi wakati ambapo inatumika katika vilabu, sehemu za
kujivinjari ama sehemu yeyote ile ambayo unaona inaweza kutumika.
Kabla
hujamsifu, ni lazima uhakikishe ni kwanini unamsifu manake mara nyingi
unapomsifu mwanamke kuhusu jambo fulani atataka kujua kwa nini
unammiminia sifa kama hizo.
Baadhi ya michongo ya kumsifu ni kama vile;
"Dress uliyoivaa imekupendeza, yaani imekufanya kuonekana mfano wa malaika"
"Una pozi lengine ajab, lazima wewe ni dansa flani"
"Nimependezwa na mtindo wako wa nguo na umbo lako, umetoklezea"
Ujanja
wa kutumia aina hii ya michongo ni kuhakikisha unacheza na tabia na
umbo lake, hakikisha kuwa unajaribu kumchunguza ili kupata mambo ambayo
anayapenda kumhusu yeye. Usisahau ya kuwa utafiti umebainisha kuwa
wanawake hupenda sana kusikia wakisifiwa.
3. Kuangazia mazingiraKulingana
na mazingira, unahitaji kuifahamu sanaa ya kuingia katika akili ya
mwanamke na kufahamu kile ambacho anafikiria. Ukifahamu kile ambacho
anafikiria, itakuwa ni jambo jema zaidi.
Kwa mfano,
kama mwanamke anajaribu kusoma lakini kila dakika anasumbuliwa na jambo
fulani, unaweza kumuuliza: "Si inaonekana ni vigumu zaidi kusoma wakati
ambapo jua ni kali zaidi huko nje?"
Kama
umekutana na kundi la wanawake na ungetaka kuanza kuongea nao, unaweza
kuwaapproach halafu useme "Nyinyi wanawake mnaonekana mnaenjoy sana na
wenye nishati, kwani kitu gani kinachoendelea ambacho nakikosa?"
Pia kama kuna mwanamke unayemzimia na hujawahi kuongea na yeye unaweza kumwambia "happy birthday"
SOMA: Mitandao 10 Maarufu Ya Kijamii Ya Kutafuta Wachumba
Michongo iliyowaziKama
wewe una confidence na unajiamini kuwa unaweza, basi njia yako ya
kutumia ni michongo iliyowazi. Kumbuka kuwa kama wakati wowote
utaonyesha unyonge katika sauti yako juwa ya kwamba michongo yako
itaanguka hapo hapo na utajiaibisha mwenyewe. [soma: Jinsi ya kumfanya
mwanamke akutamani]
Kutumia michongo
iliyowazi itakuwezesha wewe kukupatia matokeo ya haraka kwa sababu ni
kuwa wanawake hupenda wanaume ambao wanajiamini kwa mambo wanayoongea na
kufanya. Kama mwanamke ataonyesha dalili zozote za kutaka kuongea nawe
kwa njia ya miondoko ya mwili, basi unafaa kutumia michongo iliyowazi.
Baadhi ya michongo iliyowazi ni kama vile:"Unaoneka mrembo, unaweza kuniruhusu nitake kukujua zaidi?"
"Nilikuwa
nimekuona kutoka upande ule mwingine wa nyumba na nikaamua kuja
kukusalimia, bila hivyo ningeishi kujutia kukosa kumjua mwanamke mrembo
zaidi maishani mwangu"
Mwisho ni kuwa
hakikisha kuwa baada ya kutumia hii michongo kupata atenshen ya
mwanamke, hakikisha unaendeleza maongezi yenu. Jaribu kupata kulijua
jina lake halafu ujibidiishe kulitumia kila wakati, lazima atapenda.
Usisahau
kutumia sanaa za kutongoza kwa kujua vitu ambavyo mnagawa interest
pamoja, jinsi ya kumfurahisha na kadhalika. Hii utamfanya apendezwe na
wewe na mudan usiomrefunatakuzoea.
Pata mchumba, mpenzi! Click Hapa
Karibu sana msomaji wangu kila siku upate mbinu mbali mbali za kukuondolea aibu katika mahusiano yako.
Ukijenga
utamaduni wa kutembelea mtandao huu kila siku muda si mrefu unakuwa
tajiri wa mahaba pamoja na kuwa na mahusiano thabiti sana. Kazi kwako!