KONA YA UTAMU: Ushauri
Breaking News
Loading...
Showing posts with label Ushauri. Show all posts
Showing posts with label Ushauri. Show all posts

Thursday, February 16, 2017

Boss Ananitaka Kingono, Nipo Njia Panda

Image result for Boss Ananitaka Kingono
Katika harakati za kutafuta kazi nilibahatika kufika ofisi moja maeneo ya Mwenge (Dar es salaam) kwangu ilikua faraja kubwa sababu kiukweli nilikua nahangaika sana na hali ya ugumu wa maisha na sikutaka kabisa kuwa tegemezi kwa mtu yoyote (wakiwemo wazazi) niliamini kunipa elimu ni mtaji muhimu na tosha na lilikua jukumu langu kuandaa maisha yangu mwenyewe na kujitegema

Nilipofika pale niliomba kuonana na boss ila nikaambiwa haiwezekani labda ningekua na appointment, kutokana na uzoefu hii kauli nilikua nimekutana nayo mara kadhaa hivyo ilikua hainisumbui sana, nikamwambia yule receiptionist kuwa nilikua na appointment (kiukweli sikua nayo na nakiri nilidanganya na nilikosea ila sikuwa na namna mbadala) akaniuliza nimwambie we ni nani nikasema mwambie (tax consultant)

Waliongea mawili matatu then nikaruhusiwa kuingia nadiriki kusema shida ni mwalimu mkubwa sana kwani sikuwa na woga wowote kuonana na yeyote na kujinadi, baada ya mazungumzo na mahojiano ya kama dakika sita yule manager (mwanamke) akaniambia alhamisi niende nikafanye interview na kutokana na intro niliyoitoa hiyo siku (Jumanne).

Haikua kazi kwangu kupata hiyo kazi hata baada ya interview ya alhamisi, tulikubaliana terms za kazi na mshahara then nikapewa mkataba. Nilifurahi sana nikijua sasa mipango yangu itaenda vema (kwakweli mshahara ulikua mzuri tu) hadi nikaanza kupangilia biashara ndogondogo ili kuinua uchumi wangu.

Nilianza kazi wiki iliyofuata na wafanyakazi wenzangu walikua watu wema sana kwangu hivyo nilifanya kazi kwa furaha na ufanisi sana mpaka hali ilipokuja kubadilika.

MABADILIKO

Baada ya wiki moja mambo yalianza kubadilika pale ofisini, mara kwa mara boss alikua na vikao visivyokua na mbele wala nyuma na mimi na akawa mkali kwa wafanyakazi wenzangu especially wa kike na taratibu wakaanza kuniogopa.

Siku moja aliniita ofisini (ilikua Ijumaa) na akaniambia nifunge mlango nilishtuka sababu normally ukiingia ofisini lazima ufunge mlango cha kushangaza akaniambia ni-u lock nikafanya alivyotaka,

Hakuna cha maana alichoniambia zaidi ya story za kifamilia tu oooh mara mumewe (aliekuwa meneja kabla hajaumwa) anasumbuliwa na kisukari na presha na anapata taabu sana mi nikawa msikilizaji tu na aliongea muda mrefu hadi jua likazama na watu waliondoka ofisini alibaki mlinzi tu.

Aliongea mengi na mwisho akaniambia anataka nimsaidie (ngono) kitu ambacho kilinishtua kidogo ukizingatia ni mtu mzima rika la mamaangu, nilimbembeleza kuwa hapo si pahali salama ili tu aniache siku hiyo ili nikajipange jinsi ya kuepukana nae na kuikabili ile hali.

Alinikomalia sana hadi kunivamia physically na alionekana wazi alikua desperate for sex ila nilifanikiwa kumpanga na akanielewa baada ya hiyo siku ofisi nzima wakahisi nilizini na yule boss hivyo kukawa na minong'ono mingi na sikuwa na namna ya kuwaaminisha vinginevyo.

Tangu hapo ni wiki ya pili sasa huyu mama ananisumbua sana, ananiahidi mambo mengi kama nitakubali kusex nae na ni dhahiri nikimtamkia kuwa SITAKI nitapoteza kibarua kwani ye ndo meneja hapa na ndo anaajiri na kusitisha ajira,

Leo hii (Jmosi) kanipigia simu na kuniambia kesho saa saba ana kikao na mimi cha kikazi ila location naona hata aibu kuisema. Wakuu najua kuna watu humu wakike na kiume ambao wamekutana na hali kama yangu,

Naipenda kazi na sina pa kushikilia kwa sasa lakini pia sitaki kuisaliti imani yangu na msimamo kwa kupenda vitu vya dezo na kufanya uzinzi na mtu wa rika la mama yangu, ni dhambi kubwa na pia ni kinyume cha maadili ya jamii yetu lakini pia nikifikiria matokeo ya kuachishwa kazi (na mipango niliyokwisha iweka kichwani kwangu) roho inaniuma sana nabaki nikiwaza na kuwazua bila kujua haswaa nishike wapi.

Msimamo wangu ni kutokulala na huyu mama no matter the consequences ila naomba mnipe chakula cha akili ili akinifukuza kazi basi niwe nimeimarika kisaikolojia kwa ushauri wenu na nisitetereke sana kisaikolojia.

Asanteni

Wednesday, February 15, 2017

Ushauri kwa Mabinti wa Makamo Wenye Kiu na Ndoa.....

Leo nimeona nije hadharani hapa kutoa ushauri kwa mabinti wa makamo (30+yrs) ambao huenda kwa sababu za hapa na pale hawajafanikiwa kuingia kwenye ndoa wala kuwa na mahusiano yanayoashiria kuanzisha familia hivi karibuni.

Msingi wa mada yangu umetokana na mabinti kadhaa ninao kutana nao mara kwa mara maeneo mbali mbali kuwa na vilio karibu sawa.

Wakati nafanya kazi Taasisi fulani Dsm, kuna dada nilizoena nae kiasi cha kunisimulia baadhi ya mikasa ya kimahusiano na changamoto anazopitia.

Binti huyo mwenye miaka zaidi ya 30 alipitia magumu ikiwa ni pamoja na kutoa mimba kadhaa baada ya kutoona mwelekeo wa waliompachika, kuamua kugharamia mahusiano kwa kumuhudumia kila kitu mwanaume, kulazimika kubadili dini mara kadhaa kwa ajili ya mwanaume Ki uficho bila wazazi wala ndugu zake kujua.

Yote hayo aliyafanya ili kuwaridhisha wanaume angalau aitwe Mke wa fulani!! Lakini cha ajabu alikuwa anaambulia patupu

Si huyo tu, wako wengi wa namna hiyo na ambao wana visa tofauti tofauti lakini mwisho wake huishia kupata machungu na maumivu sababu ya mahusiano.

Ni kweli, ndoa ina heshima yake. Ndoa humfanya mtu aongezeke thamani katika jamii. Hilo halipingiki.

Pamoja na ukweli huo mtamu, lakini kuna ukweli mwingine ambao huenda watu hawaupendi kwamba sio wote wenye bahati ya kuwa na ndoa imara au hata hiyo ya kulega lega!! Wapo wengi wanamaisha yao mazuri na hawana hawaishi katika ndoa na wala hawajawahi kuolewa achilia mbali kutambulisha mchumba nyumbani.

Kuna mabinti wengi wanahangaika sana na wanateswa sana na mahusiano.

Unakuta Binti mzuri, mrembo, umri mkubwa tu wa kuweza kujiamlia mambo na nzuri zaidi Mungu kamjalia kazi nzuri na anauwezo wa kukabiliana na majukumu yanayohitaji pesa. Cha ajabu kutwa nzima anamaliza pesa zake kumgharamia mwanaume.

Binti huyo huyo akishika ujauzito akili hulalia upande wa kutoa eti kisa hajaolewa na anatamani sana aolewe kwani karibu rafiki zake na wadogo zake wameolewa tena kwa mbwe mbwe na michango ya harusi anatoa kila mwezi!!

Ushauri wangu ni mmoja tu, huna haja ya kuteseka wala kusononeka! Kama uwezo wa kulea unao!! Una kazi ya kukuingizia kipato, unauhakika mwanao hatokosa huduma za msingi kutoka kwako, acha kuteseka! Ruhusu moyo wako kukubali uhalisia kuwa si kila mwanamke ameandikiwa kupata watoto ndani ya ndoa. Watoto wana thamani kuliko hata hiyo ndoa unayo ng'ang'ania.

Nafahamu kuna haja za mwili za hapa na pale. Lakini ukishakuwa na maisha yako na unajitambua na kufahamu uhalisia wa maisha yako, hautashindwa kuzitimiza na kuendelea ku-control maadili ya nyumba yako!

Ni hayo tu wapwa zangu, wakuchukua achukue na wakupuuza hashikiwi fimbo!

Alamski!

SOMA: FAIDA YA KUNYONYWA UUME WAKATI WA TENDO LA NDOA

Pata mchumba, mpenzi! Click Hapa

Karibu sana msomaji wangu kila siku upate mbinu mbali mbali za kukuondolea aibu katika mahusiano yako. Ukijenga utamaduni wa kutembelea mtandao huu kila siku muda si mrefu unakuwa tajiri wa mahaba pamoja na kuwa na mahusiano thabiti sana. Kazi kwako!

Msaada: Nimeona wazazi wangu wakifanya mapenzi, je ni mkosi au laana?

Ndugu wana utamu kama mwezi uliopita nimenda kijijini kumsalimia baba na mama kwa bahati mbaya usiku mmoja hiv nilikuwa natoka nje kukojoa nilikuta mzee na bi mkubwa wakifanya yao sebuleni nikarud kimya kimya chumban kwangu wenyewe hawakuniona

Sasa mpk Leo Ile taswira inanisumbua sana nahis ni laana na mkosi sababu mambo yangu si mazur toka siku hiyo nimekuwa sijaelew kama chizi naomba msaada nifanyaje

SOMA: FAIDA YA KUNYONYWA UUME WAKATI WA TENDO LA NDOA

Pata mchumba, mpenzi! Click Hapa

Karibu sana msomaji wangu kila siku upate mbinu mbali mbali za kukuondolea aibu katika mahusiano yako. Ukijenga utamaduni wa kutembelea mtandao huu kila siku muda si mrefu unakuwa tajiri wa mahaba pamoja na kuwa na mahusiano thabiti sana. Kazi kwako!

Tuesday, December 6, 2016

NAMPENDA Mume Wangu Lakini Haniridhishi Tukiwa Faragha

Nampenda sana mume wangu lakini nimeboreka nae! in the bedroom ndio hata usiseme! yaani hata nikikaa mwezi hatujakutana siku ikitokea mechi najua kabisa anaanzia wapi atafanya nini, hayuko creative kabisa.

Najaribu kufanya changes try new positions ila yeye wala. Inaniboa! yaani I can only dream mechi za stori za sinema za x hahaha! ana mashine nzuri lakini utaalam ziro. mpaka nimenunua kitabu flani cha positions hakya nani.

Hayo yote sijawahi kucheat...ivi kuna unyago for men? nakiri kwa kweli niko shy kidogo kumpa somo, jinsi ya kuhandle mwanamke. nifanyej

Saturday, December 3, 2016

Utamgunduaje mwanamke aliekwisha zaa mtoto wakati wa mechi??

Image result for mwanamke aliyejifunguaNatumaini hali ni njema kabisa asubuhi hii wapendwa.

Natamani kupata utundu namna ya kumtambua mwanamke aliekwisha zaa mtoto/watoto kwa kutumia kiungo chake cha uzazi yani papuchi.


Inaniwia ngumu sana kuwatambua hawa unaweza kumkuta dada mdogo tuu ana mwili simple kumbe keshazaa watoto kadhaa. Kikawaida mwanamke aliezaa tumbo lake hulegea na kuwa kubwa ila wadada wa sasa sijui wanafanyaje yani wanakuwa kama sio mama kabisa.

Nataman namna ya kugundua kwa kutumia kile kiduara chetu pendwa.

USHAURI-MKE WANGU ALIWEKWA KINYUMBA NA MJOMBA WAKE

Changamoto katika maisha ya ndoa.
Ni miaka minne sasa imepita katika ndoa na huu tunaufukuzia wa tano. Ninao watoto watatu wakiwa wawili wa kike na mmoja wa kiume.
Tabia ya Mke wangu ya ukali kupita kiasi kwa wtoto ilinifanya niwe na maswali mengi sana.

Hasira hii haiishii kwa hawa vijana pekee ikawa inaenda hadi kwa ndugu zake hasa mjomba wake ambaye ndiye amemlea baada ya mama yake mkubwa kumkabidhi huko akiwa mdogo.Nilivyoona hali hii ikanibidi nmuulize taratiiibu kabisa hasahasa juu ya chuki kwa mjomba maana huwenda hawa watoto anawafunza akawa anasita kusema.

Siku nyingine alipokuwa Tayari akaamua kuniambia kuwa miaka aliyokaa na mjomba wake akisoma shule ya msingi na sekondari, MJOMBA WAKE HUYO MSHIKA DINI alimuweka kinyumba.Yaani kaka wa marehemu mama yake akaamua kuwa anambaka bintiye.

Ni zamani sana kweli na imemtokea yeye ila imi iliniumiza sana kusikia hivyo maana sikutegemea kukutana na mkasa wa aina hii.
Ukatili huu umevuka viwango vya uvumilivu.

Mjomba bado yupo.
Anajinadi kuwa ndiye aliyemsomesha.
Anadai kutambulika kwa nafasi yake ya ujomba.

Ukiwa katika nafasi hii niliyo mimi nipe maoni yako ndugu.

Thursday, December 1, 2016

Ushauri-Hivi hii inawezekana?

Habari wana kona,
Naomba kuuliza hivi inawezekana mwanamke amekuzungusha miaka 03.Kisha akakubali na akawa anaupendo wa dhati?
Eti Wadada kwa experience yenu unaweza ukamzingua mwanaume muda mrefu na yeye akawa na mapafu ya mbwa ya kukufukuzia na mwisho ukamkubali na kumkabidhi moyo wako wote bila nusunusu?
Naomba kuwasilisha.

Wednesday, November 30, 2016

Msaada jamani, Kwani ni lazima kumbebeleza mwanamke?

Kuanzia utotoni na hadi maisha ya shule nimekua katika hali ya kuyapeleka maswala yangu haraka haraka kadri ninavyotaka mimi. Katika style hiyo ya maisha imenipa faida na maendeleo mazuri.

Lakini aina hiyo ya maisha sikuwahi kabisa kumshawishi mwanamke tukaingia naye mahusiano. Nilijaribu kuwashawishi lakini walikataa wengine waliniahidi ahadi hewa. Hali hiyo haikunishutua kabisa, wasichana walionindaganya na kunikataa niliwapuuza na kuwaona ni wajinga tu. Kwani mimi nilijiona ni mume mzuri wenye kila sifa.

Na zaidi ya yote nilipohisi hali ya kufanya mapenzi nilienda kununua makahaba na kupiga masturbation. Kwa kweli katika ulimi na kinywa changu sina kabisa maneno ya kubebeleza mtu.

Maswala sasa yanakuwa magumu sana kwani hahitaji mke wa kuoa ili na mimi ni maisha yawe kama wengine na kuwa na mwanamke anayenipenda kwa hiyari yake.

Kila mwanamke ninayemfata nikajaribu kumweleza kumuoa analeta mapozi na kukataa hali ambayo inayonifanya kukataa tamaa. Na nafsi yangu huniambia huwezi kukaa ukimubebeleza mtu.

Wanawake ambao mpo humu JF naomba mnieleweshe, kwani ni lazima mbebelezwe na mpewe maneno matamu ambayo mengi ya maneno hayo ni uongo?
 

Nimetokea kumpenda sana hadi nashindwa kujicontrol

Wadau,

Nina kadent kangu ka 1st yr chuo flani hivi, haka kabinti nina muda nako naeza kukadiria ka 3 yrs.

Ofcuz kenyewe ndio kalifall in-love kipindi hiko mimi nipo college nilikua nakadharau. Sasa siku hizi kamekua M' SUPER ni kazuri kinyama.

Wakuu naeza sema kataniua kwa presha, mzee nimekuja kujikuta nina malengo nako yale ya mbalii kichizi plus na kumpenda basi ni hatarii tupu.

Somtimes naeza kukapigia simu nikakuta inatumika basi nitazila hapo, nitafikiria na mimi kulipiza kisasi cha kumpigia mtu mwingine maana najua katanicall back si nako kananipenda.

Wazee kataniuaa haka katoto nikienda nako na speed hii ambayo zamani sikua nayo.

Ushauri tafadhali.
 

Mimi black na mke wangu black mtoto kazaliwa na nywele za kiarabu

Nisaidieni wataalamu,

Hii ni siku ya tatu toka mtoto huyu azaliwe na nywele za kiarabu, leo kaja mama mkwe wamemnyoa kabla ya siku saba, nipo kimya muda wote kwa kuwa mke wangu ni mfanyakazi hawajaniomba chochote, mama yangu mzazi kafika nimemchungulia dirishani naona anamkagua sana kwa siri vipi hakuna.

DNA YA BEI RAHISI NIMALIZE FITINA.

Nioe yupi kati ya hawa? Nishaurini


Bila shaka wazima.

Kijana wenu/mwenzenu nina tatizo moja sielewi nini cha kufanya
Nilikuwa na mpenzi wangu mmoja tulipendana sana na bado nampenda sana na yeye namsifu anajua kuhandle penzi japo mapenzi yetu yameyumba kidogo kwa sasa.

Matatizo kwa kipindi chote nilichokuwa nae kiukweli (on bed) hawezi kumudu goli tatu katika tendo la ndoa, goli moja tu hataki tena na nikifanya masihara naweza kumalizia na mkono (ny*to), siwezi kulaumu kama tatizo ni yeye au mimi nakawia ku-pees, alafu kuna style ninayoipenda ya kuchuma mboga ambayo niki apply hiyo angalau nawahi kukojoa japo yeye haipendi anadai inamuumiza kizazi.

Navumilia kwa sababu nampenda siku moja nilikaa nikawaza nikasema wacha ni jaribu kutafuta mchepuko nione tatzo nini, kweli nikapata mchepuko nako yakanikuta majanga zaidi japo tofauti na ya yule ambae nampenda, nilikuwa katika majaribio lakini nikajikuta mapenzi yameamia kwake sio siri ni yupo vizuri ila dini tofauti na amenipenda sana alafu nilimdanganya sina mtu na yupo flexible kwa sexy style zote so naenjoy sana nikifanya nae mapenzi nalidhika 100%, nayeye amekubali show yangu kiasi kwamba nayeye beki hazikabi.

Mimi binafsi moyo ukawa umebeba mapenzi ya watu wawili nikiamini hawatokaa wafahamiane na isitoshe wote wakawa wanaupendo wa dhati kiasi cha kuolewa na mimi leo kesho, mwenendo huo hatukumaliza miezi mi3 mpenzi wangu wa awali akagundua kuwa nna mtu mwingine, siku simu yangu ilipigwa usiku wa kama saa tano ikapokelewa na mpenzi wangu (ni kawaida kupokea simu yangu hapo awali tuliaminiana sana kiasi cha kuwa free na simu so nikashindwa kumzuia) akakutana na sauti ya kike ghafla simu ikakata kwa kuchukia kwanini apokee mwanamke then akautuna msg akilalamika sana alaf anatabia ya kuniita mume japo hatujafunga ndoa ,
Ugomvi ukaanza hapo huyu anasema huyu nan anpiga simu usiku na anakuita mume ?

Kiukweli nilikosa majibu coz sipo vizuri kwa kujitetea kwa vitu kama hivyo ila niliyamaliza yakaisha japo hakuwa na imani tena na mimi maana dalili aliziona (mawasiliano yalipungua sana, kukutana hakukuwa kama awali ilivyokuwa hazipiti siku mbili either aje alale kwangu au nikalale kwake kibaya zaid siku akaja kwangu akakuta picha yake nillibandua ukutani bila sababu ya msingi kwake ila nilifanya hivyo ili yule mwingine asigundue lolote inshort nilielemewa na mapenzi yake so sikuwa tayari kuudhi yoyote kati yao maana kila mmoja alikuwa ana nafsi yake katika moyo wangu, mapenzi automatically yalishuka upande mmoja) na huyu mchepuko nikayamaliza akanisamehe.

Sasa nifanyaje waungwana nimejaribu kuifupisha maana visa vingi sana katikati nisiwachoshe ila kiukweli nampenda wa kwanza kwa tabia dini yake isipokuwa mapenzi (kwichikwichi zero) na mchepuko dini tofauti japo yupo radhi kubadili dini na mapenzi anayajua, ila upendo haufikii yule wa kwanza nifanye nini wadau (nata mke wa kuoa katika hao.)

NB; Mitara sitaki japo ni dini yangu inaniruhusu.

Shukrani.

Tuesday, November 29, 2016

Changamoto ya kuoa msichana mrembo sana wa kuvutia au mwenye akili sana asiyevutia

Image result for umbo namba nane
Wakuu sijui kama uzi huu umewahi kutolewa. Mara kadhaa naulizwa ushauri, inapotokea kijana wa kiume anataka kuoa kati ya msichana mrembo mwenye umbo la kuvutia sana, yaani ukitoka naye kila mwanaume atageuka kumtizama kwa kumhusudu. Ukimwona kavaa vizuri lazima usisimke mwili. Tatizo msichana mwenyewe kichwani ni mtupu sana. Mara nyingine anaongea mambo au kuuliza maswali utafikiri hajasoma, japo ana diploma ya marketing.

Upande wa pili anakuwapo msichana ambaye kwa kweli kwa sura na maumbile sio yule wa kutisha wala kushitua. Ana digrii ya BA education. Yupo kawaida sana, na sio wa kusema atakusisimua sana mwili hata kama amevaa kivipi. Na pia ana tatizo la kujipenda, ila sio mchafu, ni msafi sana tu. Kwa ujumla sio msichana wa kusema wanaume watageuka kumwangalia tena wakipishana naye au mkiwa pamoja. Ila sasa, ukiongea naye, kwa hekima na busara na kujishughulisha na kazi nyumbani yaani hakuna mfano wake. Anatoa mawazo ambayo inaonyesha anafikiri kabla ya kuongea.

Sasa huwa naulizwa; kati ya aina mbili hizi za hawa wasichana, ungechagua yupi umuoe na kuishi nae maisha yako yote; akili au urembo?

Ananiambia bikira yake imeyeyuka!

Image result for bikra
Salaam!
Habari wana kona ya utamu poleni na majukumu, mimi ni kijana ambae nimepanga kuoa mapema mwakani ila leo mchumba wangu kanitumia ujumbe unaonivuruga akili,
Kiukweli mimi na mchumba wangu hatujawahi kushiriki tendo la ndoa na alinihakikishia kuwa yeye ni bikra lakini leo kanitumia ujumbe ana wasiwasi kuwa bikra imetoka kutokana na kuhisi maumivu mara kwa mara na kazi ngumu anazofanya,

Naombeni wajuzi mnisaidie ni kweli sababu alizotoa zinaweza kusababisha bikra itoke!?

Mimi nilichomuambia bikra ikitoka asahau kuhusu ndoa!

Nifanyaje nimsahau?

Okay napenda kutoka with friends kupata one drink and two hasa every friday baada ya wiki ndefu ngumu nikishinda kazini, this day nikaamua kutokudeal na my boyfriend this weekend nkamchinjia baharini, tukaamua leo tufanye ladies day out tukaamua kuanzia kwenye happy hour sehem flan masaki right after work, wakati tukipiga story za one and two kulikua na wanaume watatu pembeni nao walikuwa wametoka kazini wakiwa bado na nguo zao za kiofisi zaidi looking smart.

My friends waliwacrush na wao walikua wakiangalia sana tulipokua tumekaa, well kiufupi nkanyanyuka kwenda toilet nkiwa narudi one of the man kati ya wale wa3 na yeye alikua anatoka washroom so akanisalimia akaomba wahamie kwa meza yetu tupige story na I said yes.

As soon as tulivofika kwenye meza zetu akawastua his friends wakahamia kweny meza yetu story story and story hadi saa tano kasoro, well wakasuggest twende night club since wao walikua na plan izo tukakubali, but tukakubaliana we shud go and change then tutameet tena saa saba katika club moja maarufu iliyoko mikocheni! My friend alichukua namba za mmoja apo na kila mtu akarudi kwake kujiandaa! Nkaamua kuvaa something sexy but classy my heels on and blah blah nikaamua ntaspend my whole weekend at my friend's place weekend nzima.. I took my stuffs ad kwake tukaamua tutumie gari lake ad eneo la tukio.


We were three and mmoja wao alidicide kutokuja kwasabb zizoeleweka basi one of my friend akawa dissapointed but yeah, we had fun this man his name felix alitokea kunilike like but mi sikuwa interested nae kabisa I had to force myself kujifanya napiga story nacheza nae but uh uh I never liked him, akaniomba namba za simu nikampa mda wa kufika kwenda nyumban tukaagana kila mtu kivyake..
Mchana naamka nkakuta missed call zake kibao na msgs nimeamkaje and blah blah nkadecide tu nsimjibu since simpendi na nini nkamchukulia poa... weekend ikaisha nkarudi kwangu my normal life style ikaendelea, akawa ananitext every morning and calls me all time nkijiskia najibu nsipojiskia haya but ye hakukata tamaa life likaendelea


Jumamosi moja my boyfriend aliamua kunitembelea ila badala ya furaha tulioshia kugombana sana sana and nkajikuta nna hasira stressed and nlikua nalia, my boyfriend aliondoka saa tano usiku akaamua kutokulala , nikiwa nimekaa naangalia tv felix as usual akanipigia akaniambia yuko na friends bar flan mikochen niende nkaona ata kama I dont like him acha niende nkapoteze mawazo, nkamuomba anifate sikujiskia kuendesha gari usiku that day, well akaja we went there story more tukaenda club tukadance morning akanirudisha nyumbani, the next day akaniomba twende beach nkenda ikawa ndo desturi most of the weekends naspend na yeye na my friends or us alone, ghafla nkajikuta naipenda campany yake, ikawa muda wa lunch mara chache anakuja kuniona.. tukawa tunaenda movies and all that..


Well.... Nlikua inlove.... tooo much inlove.... nlimpenda sana mpenzi wangu, ila kutokana na ubusy wake kwa sababu yeye ni mfanya biashara ana biashara nyingi tu, akirudi nyumbani yeye ni kula kuoga kulala hapo kalewa mkimate ni four minutes his down!! Weekend hataki kwenda popote yeye ni kulala tv tuuu au akakae bar na his friends ova! Ukimwambia bby nataka tutoke hapendi ana his own life style which is totaly different from mine... mi ni outgoing person na yeye siyo kabisa.. sio mtu wa kupiga simu mara nyingi wala kukujulia hali wala ukiwa na tatizo sio mtu wa kukishauri au kukupa pole, mkikaa hana mda wa mahaba na nini ila ivyo ivyo nilimpenda na nkaamua kuishi maisha hayo....




Felix akawa sasa my good good friend nkiwa na tatizo ntamwambia atanisaidia kwa kweli he was there for me mda wote vizawadi vya hapa na pale na alijaribu kunionyesha kwamba ananipenda ila na hayo yote sikuvutiwa naye kimapenzi, one weekend siku ya jumapili tukaamua twende kwenye band moja maarufu pale escape baada ya kuangalia band kwa mda tukaamua tusogee pemben mwa bahari tukajitenga na watu kabisa tukawa tumesimama huku tukipiga vostori, nlikua nimevaa kigaun kifupi na kiko wazi kiasi nkawa natetemeka baridi sabb ya kiupepo cha bahari akaamua kunikumbatia ghafla tukajikuta tumekiss, tulikiss mda mrefu sana almost robo saa alinikiss vizuri mpaka nkajikuta hali yangu ikawa mbaya nikitamani mengine niliamua kujikaza kikike, ndipo ulipokua mwanzo wa mahusiano yangu na yeye nikaamua kumsaliti boyfriend wangu ambaye tulidumu mwaka na miezi bila ya kumsaliti.. niliufarahia sana uhusiano wangu na felix


Yalipoanza kunikuta,
Ilikua jumatano felix aliniomba niende nkapafahamu kwake ikiwa yeye kila siku tukitaka kutoka lazima anifate kwangu kwake sikuwahi kufika, kama mpenzi wake nikakubali hapo bado sijampenda kabisa felix akinipigia napokea nsipojiskia namwambia niko busy maisha yakimawasiliano hayakua mazur sana

lakini nahisi as man alijua alichokua anakitafuta akaamua kua mvumilivu, basi nkaenda home nkajiandaa nkamwambia anifate as usual, hao adi kwake maeneo ya oysterbay, ilikua saa mbili akanipiga kitour cha nyumba yake it was a nice simple house with two bedrooms za kulala na pazuri sana, tutakaa seating room akaeka movie tukawa tunaangalia, akaamua kunikiss and nikamkiss back, the way alivyonikiss alinifanya nitake zaidi.
Ghafla akaanza kunipapasa kifuani nilijikuta simzuii nlitaka zaidi, kwa kweli alikua romantic kitu ambacho sikuwahi kuexperience kwa boyfriend wangu, alinishika shika mpaka nkajikuta nimelegea kabisa nkajikuta niko kama nilvyozaliwa alinipiga deki mpaka nkahisi kuchanganyikiwa kwa raha nilizozisikia, apo apo nkajikuta kashachomeka charger pin yake ilikua kubwa kuliko na aliichomeka taratibu

Nilisikia vitu visivyoelezeka, wakati wa show alikua akiniambia maneno ambayo yalizidi kunihamasisha wakat boyfriend wangu yeye huwa bubu anachojua ni kuchomeka charger basi, nlipewa usiku mzima hadi tukanogewa na kesho yake kila mtu aliomba ruhusa kazini.. tukaspend siku nzima tukipeana, ni vitu ambavyo sikuwahi kuvipata wala kuexperience.. aliniogesha alinifanyia massage yani nilodata kwa kweli......

Dah! Mapenzi haya yataniua

HELLO WANA MMU
naamini mu wazima wa afya...nimependa sana ku share nanyi hili suala langu na kiukweli limeanza kuniumiza kichwa na ninapoelekea nisipopata washauri makini naweza dumbukia katika tatizo ambalo litani cost maisha yangu yote..
isssue nzima inaanzia hapa

MImi ni kijana wa miaka 20 kabila langu ni mchagga pure.kwa sasa nachukulia masomo ya juu ya degree katika moja ya chuo kikuu kikubwa zaidi na maarufu zaid central and east africa.katika kuhangaikia na mambo ya ujana nilijikuta namzalisha binti mmoja ambaye nilikuwa nasoma naye.ILI kumaliza kesi kwa vile nilikuwa bado form six niliamua kumpeleka kwa mama angu akamtunza na akajifungua salama na sasa anasubiriwa mtoto akue ili na yeye aweze kurudi shule amalizie masomo yake.Kiukweli huyu binti ananipenda kutoka moyoni licha ya mjaribu yote lakini amekuwa upande wangu siku zote....na mimi nampenda sana na ndio nimeamua kabisa kutoka moyoni aje kuwa mke wangu.wazo hili limekuwa kichwani kwangu tangu natoka nyumbani mpaka nafika hapa chuoni...tena nikiwa na ahadi nikifika chuoni tu nitajitahid nipate chumba ili niishi naye mpk nitakapomaliza masomo yangu.

MAJARIBU YAMEANZA
KWA wale waliobahatika kufika chuo kikuu wanaelewa ni jinsi ghan chuo palivyo na vishawishi vingi.Na ni ukweli usiofichika kwamba chuo kikuu ndo kuna wanawake wa kila aina na warembo kupindukia.

Wiki mbili zilizopita jumanne nilikuwa naelekea lecture room kwa ajili ya kusoma.NILIPOFIKA NDANI nikakuta wanafunzi wachache akiwepo binti mmoja ambaye alikuwa amekaa upande wa mbele.ukweli wa MUNGU nilimtamani sana na nilitamani sana kama nigeweza kukaa naye karibu hata nipige naye story wakati tunamsubiria lecturer kwa vile tuliwahi nusu saa kabla..by the way nilishindwa na kuamua kupotezea na kuamua kuchezea smartphone yangu.baada ya kama dakika tano hivi nilipigiwa simu na mtu flani hv aliyekuwa akinidai pesa yake wakati nampelekea binti yule aliniita na kuniuliza kama nina ratiba kwa vile nilikuwa na haraka na ratiba ilikuwa kwa simu in form of softcopy nikawa nimemwachia na simu ili aiangalie....kwa haraka haraka nikajiongeza nikaona hii ni fursa ya kukaa na huyu binti karibu.nikamwachia na bag maksudi...then nikapelekea pesa ya watu niliyokuwa nadaiwa.nilivyorudi nikaa naye pamoja..tukaanza story za hapa na pale nikamjulia jina lake na mimi nikamwambia jina langu,,,na course tunazosomea tukaambia baada ya hapo automatically tukaanza kushare story mbalimbali za maisha kwa mfano alienda jeshini kwa hiyo akawa ananihadithia jisi kulivyo na mazoezi mbali mbali aliyopitia....kwa bahati nzuri au mbaya lecturer hakuingia kwa hiyo ikawa fursa zaidi ya kupiga naye story zaidi....binti huyu anatokea kanda ya ziwa katika eneo ambalo liliathiriwa na tetemeko la ardhi kagera....alienielezea situation nzima ilivyokuwa kwa vile alikuwepo siku tetemeko lilivyotokea ilikuwa ni story flani yenye majonz na vicheko ndani yake...baada ya kukaa naye kwa muda nilikosa kabisa njia ya kumwomba namban...baada ya muda tuliamua kuondoka mimi niliamua kuelekea library na yeye aliniaga akiniambia anaenda kula..baada ya kuondoka kama mita kumi hivi roho ilisita kabisa kuachana na yule binti bila hataa kuniachia namba kwa vile tupo wengi kumpata tena isingekuwa rahisi...nikajisemea hapana nikaahirisha kwenda library nikaamua kwenda naye kula...nikamkimbilia kwa vile hakufika mbali tukaongozana pamoja mpk cafeteria tukala kwa pamoja wali nyama wakati tukiwa mezani ndo nikapata fursa nikamwomba namba akanipatia(MISSION COMPLETE)....nikajilipia mimi pamoja na yeye akanishukuru KISHA TUKAONDOKA NIKAMSINDIKIZA MPAKA KARIBIA NA HOSTEL ALIYOKUWA anakaa..kuanzia siku hiyo nikawa na mawasiliano naye ya kiwango cha kawaida tu....jioni na mchana i akawa anipigia simu ananichukua tunaenda kula wote..mazoea yakakua zaidi ikafika kipindi akawa anachukua simu yangu kwa ajili ya kupiga picha zake kwa vile hakuja na smartphone.kabla ya kumpatia ile simu niliweka picha zangu zote katika VAULT ya application inayoitwa APPLOCK..kiufupi app hii unaweza i hide katika menu isionekane na pia ukilock application huwa kabla ujaweka password za kuunlock app ina cover ambayo huwa imeandikwa UNFORTUNATELY,APPS HAS STOPED then inajirudisha kwenye home screen kwa akili ya haraka haraka lazima utaona simu ni mbovu so nililock simu yangu apps zote za muhimu kwa style hiyo....alikaa nayo more than 24 hours kwa vile nilimwachia na na line yangu na nmba ake haikuwa kichwani na kama nilivyosema mwanzo chuon hapa tupo wengi mno so nilopezana naye kabisa after 24hrs ndo nikampata akanirudishia simu yangu huku akiilalamikia kuwa ni mbovu kwa vile kila akifungua app inagoma kabisa kufunguka...btw ukweli nilikuwa naujua mimi kuwa nilii lock kiakili...baada ya hapo ikawa joni lazima anipeleke maombi ya usiku kwa vile yeye ni mlokole ..mazoea yakapanda grade akawa ananiomba niwe napiga naye discussion.....siku moja nikiwa naye in discussion akawa ananilalamikia kuwa boyz wana mwa approach sana kiufupi wana msumbua mno akanionyesha na baadhi ya message za wanaume waliokuwa wanamsumbua akanipa simu niwajibu kirohoni nikakataa katu ila sikumwambia nilijifanya nimesahau..jioni yake tukiwa tumeenda kula akanionyesha baadhi ya boyz ambao wamemtongoza.moja ya swali gumu maishani mwangu ni kumuuliza binti kama yuko na boyfriend coz huwa akijibu ndio tu basi napoteza nguvu ya kumtongoza kabisa....basi kiujasiri nikaamuuliza bado wanakusumbua tu akanibu ndio,,, nikamuuliza sasa kwan uko mtu yeyote una ye date akaniambia ndiyo kuwa yuke na boyfriend kiukweli nilikosa pose kabisa...kwa kuvunga tu nikamwambia kama uko na boyfriend mjibu huyo msumbuaji kuwa tayari una mchumba...

nikawa nimekata tumaini la ku date naye nikajisemea rohoni huyu atabaki kuwa best friends wangu tu..kesho yake asubui akaniomba nimsubirie mchana kwa ajili ya kwenda kupata lunch kisha tukitoka hapo tuende library(katika story zangu za hapa na pale na upekuzi wake katika simu yangu alikuta baadhi picha za ofisinipamoja na sms za mahesabu mazito mazito ambako nilikuwa nafanyia kazi zamani kiufupi tu ni kwamba aligundua kuwa mimi ni bonge la mfanyabiashara kijana na katika maongezi yangu nikajikuta nimemropokea uongo kuwa nna nyumba ilhali sina chochote)baada kula pale tuliondoka tukaelekea kwa fundi nguo kisha akachukua nguo zake alizokuwa amepeleka kwa huyo fundi cherehani kwa ajili ya kuzifanyia marekebisho..kwa vile kabla ya kufika library huwa lazima tupitie kwa kwa hostel block yetu so nilimshauri kiroho safi bila nia mbaya yoyote kuwa tungezipitisha hizo nguo kwangu ili nizihifadhi kisha tukitoka library ndo tuzichukue...akanikubalia...kisha safari ya kuelekea room ikaanza tulivyofika room wote tulikuwa tumechoka choka tu bila sababu yeyote ya msingi....akaniulizia kabati langu nikamwonyesha always mara nyingi huwa naweka nguo rafu so akaamua kunisaidia kupanga nguo safi na chafu akaziweka mahala pake ake utani ukawa mwingi mara mimi navaa magauni yake aliyotoka nayo kwa fund na yeye akawa anavaa suruali zangu ...kisha akachukua nguo chafu zangu akaniambia kuwa anaenda kufua..kwa akili ya haraka haraka nikagundua kuwa safari ya library imekufa...nikachukua laptop yangu nikamwambia mimi nacheki movie kidogo akakaa tukaanza kucheki wote..filamu yenyewe ilikuwa ni ya kihindi inaitwa KAL HO NAA HO-JUNOON mhusika mkuu akiwa ni sharkuh khan tuakaa kwa pamoja tukawa tunaitazama kwa pamoja kwa kiasi flani hvi nikawa namwelewesha kwa kutumia subtitte...kwa ghafla hvi nikaanza kumwona kama vile anelegea legea hata nikiwa namwongelesha ananijibu kivivu vivu...

nikamwomba asogee ili nimwelewe movie vizuri binti huyu wa kihaya akasogea....nikajifanya kama kumwekea mkono nikaona katulia....nijisemea mwenyewe nini mbya.tukiwa tunaendelea kucheki filamu yetu mara kwa mara nikawa namshika kiuno naona kimya anajichekea tu nikaona nijiongeze nikamowmba kiss akagoma akaniambia ana boyfriend tayri nikajifanya sijasikia kabisa nikasogeza ulimi nikaona ka respond ili nisi dhalilishe wanaume wa kichagga nkasema nnahakikisha namfanyia huyu binti namfanyia mautundu yote mpaka anakufa...wakati kal ho naa hoo inaendelea siye tukawa tunaendelea na romance baadae nikafikisha mkono kunako bapo binti amechanganyikiwa analalamika kuwa yuko na boyfriend mimi sikuwaza kwa vile tulikuwa tumekaa kwa kiti nikamwomba tusogee kitandani binti wa watu akasogea.....niamchezesha match moja ya nguvu sana mpk nikawa nasumbua waliokuwa karibu na mlango na vyumba vya jirani...baada ya match akawa ananisifia mno kuwa nipo vizuri ...tukaendelea kucheki movie mpa jioni nikaenda kuoga na yeye nikamsindikiza hostel kwao kitu ambacho nilikigundua nikwamba binti alikuwa anachechemea by the way sikuwaza sana akaenda kuoga na mimi nikarudi room nikaoga jioni tukakutana tena tukaenda dinner pamoja...usiku huo huo akanitumia sms kuwa anaumia chini sana mpaka anatoka damu..mhmhmhmhmh nikamuulizia last time ume sex akaniambia one year before ,,,nikamuuliza tena na mimi ni mwanaume wake wangapi kulala naye akaniambia kuwa ni wapiliakaniambia kuwa mwanaume wake wakwanza huyo alimlazimisha sanaa lakini alivyomchomekea dushelele kwa maumivu aliyoyapata hata mshikaji hakumwaga ndani chochote akakimbia home so kwa mara ya kwanza sperm za kwanza kumwingia zilitoka kwangu kimoyo moyo nikajisemea tu kama ni kweli basi na mimi nimekula robo tatu ya bikra ake.kesho yake akniambia maumivu bado yapo nikamwambia ajikande kande labda atapona..

SHIDA INAANZIA HAPA
binti huyu amesoma shule za boarding za kanisa tangu primary..kwa maelezo yake nyumbani hata kwenda kwa jiran hathubutu lilikuwa ni kosa kubwa sana mbele macho ya mzazi..Tangu nimle binti huyu mapenzi yake yamezidi katika kiwango ambacho kimepitiliza yaani nimejikuta napendwa vile sijawahi pendwa mpaka nimejikuta mapenzi yangu kwa mke wangu yameanza kupungua kwa vile muda wote ninakuwa naye karibu kuna siku huwa nakaa naye hata mpaka saa 6 usiku tunapiga story tu....siku moja katika mazungumzo yetu nilijaribu kumuuliza vipi bado unampenda boyfriend wako akanijibu ndiyo...(..kwa vile licha ya kwamba nampenda lkn kumwoa kuna ugumu mno kutokana tayari nna mke na mtoto)nikamwomba sana asimwache awe anawasiliane sana kwa vile hayupo hapo chuoni na pia sitakuwa na kipingamizi naye chochote na nikamuahidi kutoka moyoni kuwa sintokaa nimharibie mahusiano yake na huyo jamaa ake.....na after 3 years tukishachukua degree zetu kila mtu na maisha yake...kwa kweli siku wahi mwambia kama nna mke na mtoto (nimekosa kabisa namna ya kumwambia)siku nyingine katika mazungumzo yetu na kwake nimegundua pia mapenzi yake yamepungua kwa huyo jamaa ake na nilithibishia hvyo kwamba kila wakti amekuwa akimdanganya kuwa yuko bize...upendo wake kwangu umekuwa na nguvu mno akawa ananiambia kuwa kuwa mfano nikimpa mimba hawezi kuwa tayari kutoa na wala hawezi kwenda nyumban bukoba kwa vile home kwao ni watu wenye msimamo mkali wa kidini....akaniambia kuwa mfano akipata bora nimpeleke moshi aahirishe mwaka mpaka ajifungue(kumbuka kuna siku nilishwahi mdanganya kuwa nna nyumba)jambo ambalo haliwezekani hata kidogo kwa vile moshi tayari nna mke na mtoto na wanaishi kwa mama angu..akaniambia seriously ikitokea hvyo na nikakataa bora tu ajiue....moyo ukakata ka kisu vile...kwa siku mbili tatu nimekuwa naumwa umwa yaani huyu binti ananihangaikia kama vile mme wake mpaka roommates wanionea kawivu hivi...coz muda wote wamekuwa na mimi kuniugyza matunda matunda na huduma zote za kijamii MUDA MWINGI YUPO ROOM KWANGU navyozipata zinanifanya hata akiondoka machoni kwangu dk 5 naanza ku miss..

CHANGAMOTO KUU
CHANGAMOTO YA KWANZA NI KUWA NATAMANI SANA HUYU BINTI AUJUE UKWELI KUWA TAYARI KUWA NIKO NA MTU NA NINA MTOTO NIMEJARIBU KUMWAMBIA ILA NIMESHINDWA KABISA

SHIDA YA PILI NI KWAMBA SITAKI KABISA AACHANE NA HUYO JAMAA AKE KWA SABABU NI KWAMBA TAYARI NNA MKE NA MTOTO SITOWEZA KUMUOA
nampenda mke wangu nampenda na yeye pia
....mbaya zaidi kwenye akili ya binti ameshaanza kupanga future yake na mimi
nisaidieni ushauri wa mawazo tafadhalini
 

kumbe wasichana ndivyo mlivyo!

Nna mchumba ambae kiukweli moyo wangu umelizia kumuoa.sasa kuna wakati alikuwa akitoka chuo anaelekea nyumbani huko kanda ya ziwa.alifika mwanza usiku wa nikamshauli aende kwa rafki yangu hapo mza alale kesho yake aendelee na safari

hapo kwa rafki yangu kuna kijana wa mwenye nyumba ambae pia ni kama rafki yangu japo sio kivile. sasa mchumba wangu alipokelewa na mke wa rafki yangu na wakalala pale.kesho yake mke wa rafki yangu alimsihi abaki pale hivyo hakuondoka

kijana wa mwenye nyumba akatambulishwa kuwa huyu ni mchumba wa wa fulani yani jina langu...akachangamka akapewa no ya simu na mchumba wangu...

sasa ili kuuwa soo mchumba wangu alinipigia simu akaniambia jamaa huwa wanawasiliana nae ila akasema mazoe yamezidi na eti hamuelewi kwani huwa anamtumia vocha sana bila hata kumuomba...nilimjibu we acha anisadie matumizi ...nilisema hivyo nikiamini kuwa kwa kuwa ameniambia basi hakuna kitakachotokea

basi mchumba akawa ananipa ttatifa maendeleo mala oo kaninunulia kifulushi...mara leo katuma elfu 10 ...hapo nikaanza kishtuka...wakati huo nilikuwa niko chuoni so nilipomalza ilibdi niende pale kwa rafki yangu ....hapo sasa yule jamaa akanipa xm yake iikuwa ina tazo kidogo nimlekebishie...loo gafla nikaingia kwenye sms...sikuamini macho yangu...yani kuna pesa zinatumwa nyingi kuliko nazoambiwa...kamnunulia hadi smart phone .

kituko kilikuja nilipomsitopisha mawasiliano na yule jamaa....aliniambia si ulisema akusaidie matumizi!

ujumbe wangu kwa wanaume mchumba wako akikuambia kuna mtu ananitaka usizani hampendi....anakupiga changa la macho tu