Je huu sio Udhalilishaji wa kijinsia ??? | KONA YA UTAMU
Breaking News
Loading...

Saturday, November 26, 2016

Je huu sio Udhalilishaji wa kijinsia ???

Happiness Watimanya Miss Tanzania 2013..

Swala la Shindano la Umiss kuwa halali na huku Mamiss hao wakiwa wanaonekana wakiwa uchi (Wakitembea na Vichupi) pindi wanapokuwa Jukwaani.. Je Huu sio Udhalilishaji ???


Shindano la Umiss ni shindano ambalo  limebarikiwa na Wizara ya Michezo na Utamaduni Kupitia taasisi ya BASATA kuwa ni halali na imekuwa sio Dhambi wala sio kosa kisheria Pindi tunapowaona Mamiss hao wakitembea Jukwaani na Vichupi ila chakushangaza jambo hilo hilo likifanyika katika mitandao ya kijamii au katika Video za kisanaa kama Bongo Muvi au Video za muziki wa Bongo Fleva utaambiwa huu niudhalilishaji wa kijinsia na nikosa kisheria....
Miss Universe Tanzania 2014 Nale Boniface..
SWALI kwa BASATA je Sheria inayokataza Udhalilishaji wa kijinsia Katika Video za sanaa hapa nchini ni tofauti na hii ya mamiss kutembea na Vichupi jukwaani tena mbele za watu ???

TUJIKUMBUSHE MATUKIO YA NYUMA
Mwaka jana ilitokea skendo ya Mwanamuziki wa kike SHILOLE kufungiwa na BASATA kosa la kucheza uchi mbele za watu katika shoo yake iliyo fanyika katika nchi ya Ubelgiji Tarehe 9 May 2015.

Picha za tukio hilo ambazo zilimgharimu Shilole kufungiwa kwa mwaka mmoja bila kujishuhulisha na sanaa, japokuwa alifutiwa adhabu hiyo.
Hii ni Picha ya Video ya ZIGO ya AY na DIAMOND ambayo na yenyewe pia imefungiwa na BASATA kwa kukosa maadili ya kijamii na udhalilishaji wa kijinsia.

Lakini pia kuna Video za wasanii kutoka nje ya Tanzania ambazo hazina maadili kijamii na zinaudhalilishaji wa kijinsia lakini zinapigwa kwenye TV zetu kilasiku na hata siku moja BASATA hawajazitolea tamko wala kuzipiga marufuku zisionyeshwa..

HUU NI MSIMAMO WA BASATA AMBAO ULITOLEWA MWAKA 23/9/2015
BASATA wametoa siku saba kwa wamiliki wa wavuti, na wale wenye akaunti kwenye mitandao ya kijamii Kuondoa nyimbo zenye kusambaza chuki, matusi, kashfa, kejeli na udhalilishaji wa watu wa kada mbalimbali wakiwemo wanasiasa.

Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza, amevitaka pia vyombo vya habari ikiwamo redio, luninga, kuondoa na kuacha mara moja kucheza au kurusha nyimbo zote zenye maudhui hayo.

PICHA ZA MAMISS WETU WAKIWA NA VICHUPI MAJUKWAANI..








Pata mchumba, mpenzi! Click Hapa
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT